Amesafiri nchi nyingine ambayo wametofautiana mwezi mwandamao

Swali: Mwenye kufunga siku ishirini na nane kisha akasafiri nchi nyingine ambapo kwao mwezi mwandamao wa Shawwaal umethibiti kuingia – afanye nini? Lini afunge siku hiyo ambayo amebaki anadaiwa?

Jibu: Akisafiri kabla ya siku ishirini na tisa kisha akafika katika nchi nyingine hali ya kuwa ni msafiri ilihali wao wamefunga, basi atatakiwa kufunga pamoja nao. Na ikiwa wao hawakufunga basi atafungua pamoja nao. Hakuna utatizi katika hili. Halafu baadaye atalipa siku moja baada ya siku ya idi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´laam-ul-Musaafiriyn, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 01/06/2019