Amesafika na hedhi lakini haoni mtiririko mweupe ukitoka

Swali: Ni ipi hukumu damu ya mwanamke ikikatika baada ya ada ya mwezi? Je, inazingatiwa ni kutwaharika pamoja na kwamba hajaona al-Qaswah al-Baydhwaa´?

Jibu: al-Qaswah al-Baydhwaa´ inakuja pale damu inapokatika. Kwa sababu damu inapokatika mwanamke hutokwa na mtiririko mweupe na hahisi tena kutokwa na damu. Hii ndio “al-Qaswah al-Baydhwaa´”. Kujengea juu ya hili pale damu/hedhi ya mwanamke inapokatika basi mwanamke amesafika na hapo swalah na swawm itakuwa ni wajibu kwake. Vilevile itafaa kwa mume wake kumjamii ikiwa yuko na mume.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1640
  • Imechapishwa: 31/03/2020