Amepuuza kutoa zakaah kwa miaka mingi

Swali: Kuna mtu alichukulia wepesi suala la kutoa zakaah kwa miaka mingi. Hivi sasa baada ya kutubia analazimika kutoa ile miaka iliyompita au inatosha kutubia?

Jibu: Hapana, tawbah haitoshi. Ni lazima kutoa zakaah. Ni wajibu kwake kutoa juu ya ile miaka iliyompita pamoja na kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (91) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-22-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 10/08/2018