Amepoteana na Mahram wake mahali pa kurusha vijiwe

Swali: Kuna mwanamke amepoteana na Mahram wake sehemu ya kurusha vijiwe, jambo lilisababisha akashindwa kurusha vijiwe. Akamuwakilisha mtu asiyemjua amrushie vijiwe. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ikiwa mtu huyo ni mwaminifu hapana ubaya akawakilisha mtu amrushie vijiwe kwa sababu yeye katika hali kama hii hawezi. Lakini endapo angelichelewesha kurusha vijiwe mpaka pale atapompata Mahram wake ambapo akaenda naye na akajirushia vijiwe mwenyewe, ingelikuwa bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1410
  • Imechapishwa: 14/12/2019