Ameporomosha mimba ya miezi miwili kwa kutokukusudia

Swali: Mwanamke huyu ada yake ya kila mwezi imekatika sasa ni miezi miwili. Alikuwa na ujauzito. Alikuwa hajui kuwa ni mjamzito kwa sababu ya kutokujua kwake viashirio vya mimba. Akahisi uzito na vibaya tumboni mwake ambapo akatumia dawa za kumfanyia wepesi ilihali hajui kuwa yuko na mimba. Alitumia dawa hiyo kama tiba tu. Matokeo yake mimba yake ikaporomoka. Baada ya Allaah kumruzuku kizazi na wadogo wanasoma chuo kikuu na hayo yametokea miaka thelathini huko nyuma. Je, amepata dhambi au juu yake ana kafara kwa aliyofanya pamoja na ujinga wake na hapo kabla alikuwa hana mwanachuoni wala Mashaykh wa kuwauliza?

Jibu: Hakuna juu yake kitu. Kwa sababu mimba hii alikuwa bado hajakuwa mtu. Jengine ni kwamba hakunywa dawa kwa lengo la kuiporomosha mimba hii. Alikunywa ili kujifanyia wepesi tumbo lake kwa kule kufikiria kwake hiyo ni dawa ya tumbo. Kwa hivyo juu yake hakuna kitu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1415
  • Imechapishwa: 21/12/2019