Amepona baada ya kuwa na maradhi yasiyotarajiwa kupona

Swali: Mtu akipona kutokamana na maradhi ambayo madaktari walitangulia kumthibitishia kuwa hawezi kupona na hayo yamepitika baada ya kupita masiku kadhaa ya Ramadhaa. Je, anatakiwa kuombwa kuyalipa masiku hayo yaliyompita?

Jibu: Mtu akila Ramadhaan nzima au baadhi ya siku za Ramadhaan kwa sababu ya maradhi yasiyotarajiwa kupona ima kwa sababu ya kawaida au kwa sababu ya mathibitisho ya madaktari waaminifu, basi lililo la wajibu kwake ni kulisha kwa kila siku moja masikini. Akifanya hivo na Allaah huko baadaye akamkadiria kupona basi sio lazima kwake kufunga yale masiku aliyotoa chakula. Dhimma yake imetakasika kutokamana na kile chakula alichotoa badala ya kufunga. Ikiwa dhimma yake imetakasika basi hakuna uwajibu unaomgusa baada ya kutakasika dhimma yake.

Mfano wa haya ni yale yaliyotajwa na wanachuoni wa Fiq juu ya mtu asiyeweza kutekeleza faradhi ya hajj kutokuweza ambako hakutarajiwi kuondoka, akawakilisha mtu amuhijie kisha baadaye akaweza, haimlazimu kutekeleza faradhi hii kwa mara ya pili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/126-127)
  • Imechapishwa: 21/06/2017