Amepitwa na Takbiyr za swalah ya ´Iyd

Swali: Mtu afanye nini akipitwa na Takbiyr ya Rak´ah ya kwanza ya swalah ya ´Iyd? Je, ailipe?

Jibu: Hapana. Imeshampita.

Swali: Rak´ah ya kwanza ikimpita?

Jibu: Aiswali kawaida kama ilivyo kwa Takbiyraat zake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (14) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-03-11-1434.mp3
  • Imechapishwa: 29/05/2019