Amepangusa soksi moja na mguu mwingine akaosha


Swali: Mtu akifuta kwenye khofu zake kisha akavua moja wapo. Halafu baada ya hapo akapatwa na hadathi ambapo akawa amefuta moja wapo na akaosha kawaida mguu wake mwingine na akawa ameswali kwa namna hii kwa sababu kwenye ule mguu mwingine ambao hakuvua ilikuwa imechanika. Mtu huyu alikuwa hajui hukumu. Je, azirudi swalah zake alizoswali? Afanye nini ikiwa hajui ni swalah ngapi alizoswali kwa namna hii?

Jibu: Akipangusa juu ya khofu mbili kisha akavua moja wapo, wudhuu´ wake unabatilika. Hivyo atatakiwa kutawadha upya. Ikiwa aliswali basi anatakiwa kuzirudi kwa mpangilio. Ikiwa hajui ni ngapi, basi aswali kwa kiasi cha vile anavyodhania. Ikiwa ana dhana yenye nguvu kwamba ni swalah kumi, ishirini au thelathini, basi atenge wakati wa mchana na aziswali. Hafai kwake kuchelewesha Dhuhr akaiswali pamoja na ´Aswr au akaswali ´Aswr pamoja na ´Aswr nyingine. Aziswali zote kwa pamoja kwa mpangilio kwa njia ya kwamba aanze na Fajr, Dhurh, ´Aswr, Maghrib kisha ´Ishaa. Isipokuwa ikiwa swalah hizo ni nyingi na muda wake umeshakuwa mrefu, huyu ni wajibu kwake kutubu kwa Allaah na awe na msimamo huko mbeleni. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumuamrisha yule mbedui ambaye alikuwa akidonoa swalah zake kama jogo azirudi swalah hizo zilizokuwa nyingi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2018