Ameona utoko kwenye nguo na hakumbuki kuwa usiku aliota


Swali: Baada ya kuamka mtu akiona utoko usiyozidi matone nne unaonukia manii lakini hata hivyo hakumbuki kuwa aliota. Je, aoge?

Jibu: Uwajibu wa kuoga haikushurutishwa mtu akumbuke kuwa aliota. Hata kama mtu hakumbuki kuwa aliota akihakikisha kuwa ni manii. Ama akihakikisha kuwa sio manii na kwamba ni madhiy, basi aoshe dhakari au uke wake na aoshe kile kilichopatwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 06/04/2018