Amenyanyua kichwa kutoka Sujuud kwa kusahau

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusujudu na akanyanyua kichwa chake kutoka kwenye Sujuud kwa kusahau?

Jibu: Ni lazima kwa mtu kuweka [paji la uso] juu ya ardhi mwanzoni mwa kusujudu mpaka mwishoni mwake. Ni lazima vilevile mtu asujudie juu yake mwanzoni mwake na mwishoni mwake. Akisujudu juu yake mwanzoni mwa Sujuud kisha akainuka mwishoni mwake anakuwa amesujudu juu yake. Akisujudu na akatulizana basi kumepatikana kile kinachotakikana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 24
  • Imechapishwa: 17/07/2018