Amenuia usiku atafunga kesho damu yake ikikatika


Swali: Kuna mwanamke alijiwa na ada yake ya mwezi katika Ramadhaan. Ile siku ya mwisho ya hedhi akalala usiku na bado akawa hajatwaharika ambapo akanuia akisafika basi atafunga. Lakini hata hivyo hakusafika isipokuwa baada ya Fajr. Akatazama akaona kuwa amesafika. Je, akamilishe swawm yake na inakuwa sahihi au alipe siku nyingine badala yake?

Jibu: Afunge siku nyingine badala yake. Hilo ni kwa sababu alilala akiwa na mashaka kwenye nia yake ambapo hakuwa anajua kama kizuizi cha swawm – ambacho ni hedhi – kitaondoka au hakitoondoka. Kwa hivyo ni wajibu kwake kulipa badala ya siku ile. Ikiwa siku ile alifunga atalipwa kwa nia yake. Vinginevyo dhimma yake haitakasiki isipokuwa kwa kulipa siku ile.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/924
  • Imechapishwa: 06/06/2018