Amemwingilia mke wake siku aliokuwa akilipa Ramadhaan

Swali: Kuna mtu alikuwa akilipa deni lake la Ramadhaan katika Shawwaal ya mwaka 1410. Mke wake akajionyesha kwake ambaye alikuwa hakufunga. Mtu huyo hakuweza kuimiliki nafsi yake ambapo akamwingilia.

Jibu: Ni wajibu kwa ambaye amefungua katika isiyokuwa Ramadhaan alipe siku nyingine badala ya siku hiyo aliyoiharibu kwa sababu ya jimaa. Halazimiki kutoa kafara kwa sababu jimaa haikutokea katika Ramadhaan. Ni wajibu kwako kutubu kwa Allaah kutokana na hilo. Kadhalika mke ni wajibu kwake kutubu kutokana na hilo kwa sababu yeye kasababisha kukufunguza.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/319)
  • Imechapishwa: 17/06/2017