Amemwingilia mke wake akidhani kuwa bado hakujapambazuka

Swali: Kuna mtu amemwingilia mke wake katika usiku wa Ramadhaan huku akidhani kuwa bado hakujapambazuka. Baada ya kumaliza kazi yake akatoka chumbani kwake na ikambanikia kuwa amefanya jimaa baada ya daku ambapo akajuta na kutimiza siku yake. Lakini hata hivyo anahisi kupata dhambi na anauliza kitendo chake kinapelekea katika nini?

Jibu: Mambo yakiwa kama alivyosema basi ni wajibu kwake kulipa siku hiyo ikiwa imembainikia kuwa jimaa imetokea baada ya uwajibu wa kujizuia ambapo ni kwa kule alfajiri kuingia. Anawajibika vilevile kutoa kafara ambayo ni kuacha mtumwa muumini huru, asipopata anatakiwa kufunga miezi miwili mfululizo, asipoweza anatakiwa kulisha masikini sitini. Kafara hiyo ni kwa sababu ya kuchukulia kwake wepesi kutotaka kujua kuwa alfajiri imeshaingia. Haya yanamuhusu vilevile mke wake midhali hakulazimishwa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/317)
  • Imechapishwa: 17/06/2017