Amemnyonyesha mtumzima ili awe Mahram yake


Swali 994: Kuna mwanamke ambaye hana Mahram na anataka kusafiri kwenda nchini mwake. Akamnyonyesha mwanaume maziwa kwenye kikombe. Je, maziwa haya yanamfanya kuwa Mahram wake?

Jibu: Hayamfanyi kuwa ni Mahram wake. Maziwa yanayofanya uharamu ni yale yanayokuwa ndani ya miaka miwili. Ama kumnyonyesha mtu mkubwa unyonyeshaji huo hauna athari yoyote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 394
  • Imechapishwa: 18/08/2019