Amemjamii mkewe mchana wa Ramadhaan na hawezi kufunga kwa sababu ya kazi

Swali: Nimemjamii mke wangu mchana wa Ramadhaan. Lakini siwezi kufunga kwa sababu mimi ni mfanyakazi. Je, kuna kafara zengine?

Jibu: Ndio, kuna kafara zengine kukiwemo kulisha masikini sitini. Yule anayemjamii mke wake mchana wa Ramadhaan katika mji wake ni lazima kwake kuacha mtumwa huru, asipopata basi afunge miezi miwili mfululizo, asipoweza basi alishe masikini sitini. Ama akimjamii katika usiokuwa mji wake, kama kwa mfano mwanaume aliyesafiri kwenda ´Umrah ilihali yeye na mke wake wamefunga, kisha akaanza kumjamii katika safari hii – ni mamoja njiani au Makkah – hakuna neno. Haijalishi kitu hata kama atataka kubaki mwezi mzima wa Ramadhaan. Kwa sababu msafiri halazimiki kufunga.

Nasaha zangu ni kwamba mtu anatakiwa kumcha Allaah (´Azza wa Jall) na asiibadilishe neema ya Allaah ikawa kufuru. Allaah kamneemesha mke. Hivyo hatakiwi kufanya ikawa ni sababu ya kuyaendea yale aliyoharamisha Allaah kwa kumwingilia mchana wa Ramadhaan. Kuna mtu alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akamwambia:

“Nimeangamia.” Akasema: “Nimemwingilia mke wangu katika Ramadhaan ilihali nimefunga.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamkubalia maneno yake kwamba ameangamia kweli na akafanya kitendo hichi ni kuangamia kweli. Usiku uko karibu. Anaweza kumwingilia nusu ya mchana na hakuna kilichobaki kwake isipokuwa nusu nyingine au akamwingilia mwanzoni mwa mchana na hakuna kilichobaki kwake isipokuwa mchana uliobaki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (59) http://binothaimeen.net/content/1346
  • Imechapishwa: 20/11/2019