Amembusu mke wake akatokwa na madhiy mchana wa Ramadhaan


Swali: Kuna mtu amembusu mke wake mchana wa Ramadhaan ambapo akawa ametokwa na madhiy. Je, swawm yake inaharibika?

Jibu: Kutokwa na madhiy peke yake hakuharibu swawm. Kama ni madhiy peke yake ndio yametoka hayaharibu swawm. Kinachoharibu swawm ni kutokwa na manii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaam al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 02/06/2017