Amemaliza I´tikaaf yake kwa kufuata mwezi mwandamo wa nchi nyingine

Swali: Mimi ni katika wakazi wa Kuwait na katika kumi la mwisho la Ramadhaan nilikuwa mwenye kukaa I´tikaaf. Nilivunja I´tikaaf yangu na kwenda nyumbani kwangu, nikamjamii mke wangu na nikafungua baada ya kujua kuwa umethibiti mwezi mwandamo Saudi Arabia na nchi nyenginezo. Kwa sababu nilidhani kuwa siku hiyo ni Shawwaal na wala haijuzu kufunga ndani yake. Ni ipi hukumu ya ki-Shari´ah juu ya suala hili juu yangu na kwa mke wangu?

Jibu: Umepatia kufungua siku ya ijumaa na kutoka nje ya I´tikaaf yako. Kwa sababu ni siku ya ´Iyd kwa kuthibiti mwezi mwandamo wa Shawwaal usiku wa kuamkia ijumaa. Imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´álayhi wa sallam) amesema:

“Fungeni kwa kuuona na fungueni kwa kuuona.”

Ikiwa idadi ya siku ulizofunga za Ramadhaan ni ishirini na nne basi unatakiwa kulipa siku moja ili zitimie siku ishirini na tisa.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin al-Ghudayyaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/413) nr. (7886)
  • Imechapishwa: 25/04/2022