Amelazimishwa kushiriki kazi za jeshini na yeye anataka kuhiji

Swali: Kuna mtu anafanya kazi jeshini na analazimika kufanya hajj kwani bado hajahiji. Anataka kuitekeleza mwaka huu lakini hata hivyo amelazimishwa kushiriki katika kuwahudumia mahujaji. Je, ni lazima kwake kukataa na kuhiji?

Jibu: Si lazima kwake kukataa. Bali anachotakiwa ni yeye kusikiliza na kutii. Wakati fulani wanaombwa kushiriki lakini hata hivyo wanaweza kupewa ruhusa siku ya ´Arafah kuhirimia hajj. Akiruhusiwa siku ya ´Arafah kuhirimia hajj basi ahirimie kuanzia ´Arafah. Si lazima kwake kwenda miyqaat. Kwa sababu hakuwa na uwezo wa kuanza ´ibaadah za hajj isipokuwa katika maeneo haya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye ni wenye mawaaqiyt ni pale atakapoanzia.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1570
  • Imechapishwa: 06/03/2020