Amekwepa adhabu katika nchi ya Kiislamu na akatubia

Swali: Kuna mtu anaishi katika nchi inayohukumu kwa sheria za wanadamu kisha akatoka na hakukatwa mkono wake na baadaye akatubu. Ni kipi cha wajibu hivi sasa?

Jibu: Hata kama atakuwa katika nchi ya waislamu ambapo wanakata mikono. Akitubu kwa Allaah kabla ya jambo lake kupelekwa serikalini basi Allaah anamsamehe. Kule kutubu na kuisitiri nafsi yake ndio bora. Lakini pamoja na kutubia anatakiwa kurudisha haki kwa mmiliki na amuombe msamaha. Lakini kama ameshafika kwa mtawala ni lazima atekelezewe hukumu ya Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam https://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/04.mp3
  • Imechapishwa: 17/11/2018