Swali: Mfungaji akisukutua kinywa chake au akapandisha maji puani na maji yakaingia tumboni mwake. Je, swawm yake inaharibika?

Jibu: Hapana, kwa sababu hakukusudia kufanya hivo. Amesema (Ta´ala):

وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُم بِهِ وَلَـٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ

”Hapana dhambi juu yenu katika yale mliyoyakosea, lakini isipokuwa katika yale yaliyoyakusudia nyoyo zenu.”[1]

[1] 33:05

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/290)
  • Imechapishwa: 25/05/2019