Amekumbuka swalah zilizopita masiku kadhaa

Swali: Nilikuwa nasafiri kwa ndege na nilikuwa na janaba. Sikupata kitu cha kufanyia Tayammum. Matokeo yake swalah ya Dhuhr, ´Aswr na Maghrib zikanipita. Nilipofika al-Madiynah nikaoga janaba ambapo nikawa nimewahi swalah ya ´Ishaa katika mkusanyiko na akasahau kulipa hizo swalah zengine. Kukapita masiku kadhaa ndipo akawa amekumbuka. Ni lipi la wajibu kwake?

Jibu: Anatakiwa azilipe. Ni lazima azilipe. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kusahau swalah au akapitikiwa na usingizi, basi aziswali pale atapokumbuka. Hana kafara nyingine isipokuwa hiyo.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (81) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-1-3-1439-01.mp3
  • Imechapishwa: 01/04/2018