Amekumbuka kuwa yuko na kitambara cha najisi ndani ya swalah

Swali: Nilikuwa na kitambara kilicho na najisi ambacho nilikiweka mfukoni mwangu ili baadaye nikitupa kwenye taka. Lakini nikasahau na nikakumbukam ndani ya swalah. Je, ni lazima kwangu kuikata swalah au niendelee kuswali?

Jibu: Usikate swalah yako. Kitoe kitambara hicho chenye najisi ndani ya mfuko na kiweke mbele yako ardhini. Pindi utakapotoa salamu utakichukua. Hii ndio Sunnah kwa yule mwenye kujua katikati ya swalah kwamba yuko na nguo au kitu chenye najisi. Anatakiwa kujikwamua nacho na kuikamilisha swalah yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (98) https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18006
  • Imechapishwa: 14/05/2019