Amekumbuka Kuwa Hakuweka Nia Katikati Ya Swalah


Swali: Mswaliji akisahau kuweka nia na akaikumbuka katikati ya swalah inatosha kule kuileta katika hali hii?

Jibu: Ni vipi amekuja akatawadha, akasimama na kuswali bila ya kuweka nia? Hii ni dalili yenye kuonyesha kuwa aliweka nia. Haitakiwi kuwa na wasiwasi. Kule kutia kwake wudhuu´, kuja kwake, kusimama kwake na kuleta kwake Takbiyr ni dalili inayoonyesha kuwa aliweka nia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (9) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt--14340506.mp3
  • Imechapishwa: 16/04/2017