Amekumbuka kuwa ana deni la Ramadhaan baada ya kuingia Ramadhaan nyingine

Swali: Nilisafiri katika Ramadhaan na nikala siku mbili ambazo nilinuia kuzifunga. Lakini sikuyakumbuka hayo isipokuwa baada ya kuingia Ramadhaan ya mwaka huu.

Jibu: Uhalisia ikiwa ni kama ulivosema basi huna dhambi kwa kuchelewesha siku mbili ulizokula mpaka kukaingia Ramadhaan nyingine. Unalazimika kuzilipa baada ya hapo. Imethibiti ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema ya kwamba Allaah (Subhaanah) amesema:

“Nimekwishafanya.”[1]

Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake:

“Atakayesahau na akala au kunywa basi atimize swawm yake. Kwani si vingine ni Allaah ndiye kamlisha na kumnywesha.”[2]

[1] 02:286

[2] al-Bukhaariy (1933), Muslim (1155), at-Tirmidhiy (721) na wengineo.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/336-337)
  • Imechapishwa: 18/06/2017