Amekumbuka kuwa aliswali na janaba

Swali: Kuna mtu ameswali Dhuhr, ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa. Siku ya pili akagundua kuwa aliswali hali ya kuwa na janaba. Je, arudi kuswali swalah hizo?

Jibu: Ndio, swalah zote ambazo aliswali bila ya kuoga janaba ni wajibu azirudi kwa kuwa sio sahihi. Hapa ni pale ambapo ikiwa ndoto yake alitokwa na manii. Ama ikiwa aliota bila ya kutokwa na kitu, hahitajii kuoga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Maji yanatokamana na maji.”

Hili linahusiana na kuota.

Mwenye kuota jimaa usingizini akiona athari ametokwa na kitu anatakiwa kuoga. Ikiwa hakuona kitu kimechotoka, hahitajii kuoga.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2105
  • Imechapishwa: 30/06/2020