Swali: Mwenye kukumbuka baada ya kuswali kuwa alikula nyama ya ngamia ni lazima arudi kuswali?

Jibu: Ndio, kwa kuwa Wudhuu wake umetenguka kwa kula nyama ya ngamia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa:

“Je, mtu atawadhe kwa (kula) nyama ya ngamia?” Akasema: “Ndio.”

Akikumbuka kuwa alikula na hakutawadha baada ya kula nyama ya ngamia anatakiwa kutawadha na kurudi kuswali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf-1432-07-05.mp3
  • Imechapishwa: 24/04/2018