Amekumbuka ameacha nguzo baada ya swalah


Swali: Mwenye kusahau nguzo miongoni mwa nguzo za swalah na akaikumbuka baada ya muda mrefu au mfupi, afanye nini?

Jibu: Akiikumbuka karibuni, ni sawa na kuacha Rak´ah nzima. Hivyo, asimame na kuleta Rak´ah hiyo moja na asujudu Sujuud-us-Sahuw. Ama akiikumbuka baada ya muda mwingi au Wudhuu wake ukatanguka, arudi swalah kuanzia mwanzo wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (43) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-03-17.MP3
  • Imechapishwa: 16/11/2014