Amekumbuka ameacha jambo la wajibu baada ya swalah

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kuacha jambo la wajibu miongoni mwa mambo ya wajibu katika Swalah ikiwa ni kwa wakati wa karibu tu na vipi ikiwa kumeshapita wakati mrefu?

Jibu: Akiacha jambo la wajibu miongoni mwa mambo ya wajibu kwa sahau, asujudu Sujuud-us-Sahuw. Ikiwa ameshatoa Salaam, basi asujudu baada ya kutoa Salaam. Isipokuwa ikiwa kama Wudhuu wake utakatika baada ya kutoa Salaam au kumeshapita muda mrefu, katika hali hii Sujuud-us-Sahuw kwake imebomoka (hana Sujuud-us-Sahuw).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (45) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-03-24_0.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014