Amekula siku tatu za Ramadhaan kwa makusudi


Swali: Nilikula katika Ramadhaan kwa kukusudia kwa siku tatu na inaweza kuwa zaidi ya hapo. Kisha nikatubu kwa Allaah. Ni lipi la wajibu kwangu?

Jibu: Ni wajibu kulipa masiku haya matatu ambayo ulikula ikiwa ulikula mchana wa Ramadhaan. Ama ikiwa tokea mwanzo wa siku ulikuwa hukufunga  basi hayatokubalika kutoka kwako japokuwa utayalipa. Lakini ni juu yako kutubu kwa Allaah na ukithirishe matendo mema.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/931
  • Imechapishwa: 07/05/2018