Amekufa baada ya kutambulika kutamka maneno ya kufuru

Swali: Kuna mtu alikuwa akitambulika kutamka maneno ya kikafiri. Abainishiwa hoja halafu akafa pamoja na kwamba anajulikana kwa maneno mengine yanayopingana na yale maneno yaliyosemwa juu yake ya kikafiri. Je, kusemwe kuwa alikufa na pengine alitubia kwa Allaah (Ta´ala) kabla kufa kwake au ahukumiwe kwa dhahiri?

Jibu: Anazingatiwa kuwa ni muislamu kama wengine midhali kumepokelewa kutoka kwake maneno yanayoweza kueleweka hivi na vile. Kimsingi huyu ni muislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 23/01/2018