Amekufa akiwa na deni la Ramadhaan baada ya kuwa na maradhi yasiyotarajiwa kupona

Swali: Mamangu aliuguwa siku tisa kabla ya Ramadhaan. Ramadhaan ilipita siku tano kisha akafariki. Je, swawm ni yenye kumuwajibikia au hapana?

Jibu: Ikiwa inahusiana na maradhi yasiyotarajiwa kupona basi anatakiwa kutolewe chakula kwa kila siku moja kumpa masikini. Kwa sababu kila mtu ambaye imemfikia Ramadhaan na yeye ana maradhi yasiyotarajiwa kupona anatakiwa kulisha kwa kila siku moja masikini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/116)
  • Imechapishwa: 18/06/2017