Swali: Mimi ni kijana niliyeoa. Nilichuua mkopo wa Riyaal 1000 na baadaye nirudishe Riyaal 1050 kwa ajili ya kutoa mahari pamoja na kuzingatia kwamba nina watoto. Ni ipi hukumu ya ndoa yangu? Ni kipi cha wajibu ninachotakiwa kufanya?

Jibu: Kuhusu ndoa ni sahihi midhali imetimiza masharti yake. Kuhusu kukopa Riyaal 1000 na baadaye kurudisha Riyaal 1050 ni ribaa. Ni haramu. Ni wajibu kwako kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) kutokana na ulichokifanya. Ikiwa tayari ameshamlipa mwenye deni lake, basi ni wajibu kwake kutubia na aazimie kutorudi kufanya kitu kama hicho. Ama ikiwa bado hajamlipa ile ribaa mwenye nayo, basi anatakiwa kurudi na kupata na mpokeaji wa ribaa hiyo. Akirudi mahakamani basi mahakama wana maoni yaliyo na kheri ndani yake – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (48) http://binothaimeen.net/content/1110
  • Imechapishwa: 11/04/2019