Swali: Inajuzu kwa mume kumkataza mke wake kuwatembelea na kuwatendea wema ndugu zake? Ni manaswara na wanaishi nje ya nchi hii.

Jibu: Asimkataze kuwatembelea ndugu zake hata kama ni manaswara. Yeye kukutana nao ni katika wema. Asimkataze kuwatendea wema wazazi wake:

وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖوَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا

“Lakini wakikung´ang´ania kwamba unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii na tangamana nao kwa wema duniani.” (31:15)

Mzazi kafiri ana haki ya kutendewa wema na mtoto wake muislamu. Hata hivyo asimpende. Amtendee wema na wala asimpende. Anatakiwa kurudisha wema kutokana na juhudi alizotoa kwake, kumlea na kumhudumia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (68) http://alfawzan.af.org.sa/node/16495
  • Imechapishwa: 26/08/2017