Amekata swalah kwa harufu mbaya aliyeko pambizoni mwake


Swali: Je, mtu anapewa udhuru wa kukata swalah yake kwa kupatikana harufu mbaya kutoka kwa mmoja katika waswaliji pambizoni mwake ikiwa inamuharibia unyenyekevu wake?

Jibu: Ikiwa hawezi kustahamilia hilo basi:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

”Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[1]

Baadhi ya watu hawawezi kustahamilia hilo. Nimeambiwa na baadhi ya watu kwamba wamefanya hivo. Ikiwa hawezi kustahamilia hilo na unyenyekevu wake ukaondoka basi anakuwa ni mwenye kupewa udhuru kwa jambo hilo. Dhambi zinampata huyo aliyeko pambizoni mwake.

[1] 02:286

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (21)
  • Imechapishwa: 13/08/2021