Amekasirishwa na kitendo cha nduguye kumuozesha msichana wake bubu

Swali: Mimi nina ndugu ambaye amemuozesha dada yake kwa mwanaume ambaye ni bubu. Mwanamke yeye na familia yake si bubu. Mume huyu anaswali na hatumtuhumu kwa kitu chochote katika dini yake. Mimi tu ndiye nimekasirishwa na kitendo hicho na nikasema kwamba kitendo hichi si katika ufanisi, kwani familia nzima imesalimika na jambo hilo. Shaytwaan ananijia na kunambia kwamba niko katika haki ambapo nazidi kukasirika zaidi. Je, hili linaiathiri dini yangu pamoja na kuzingatia ya kwamba mke hivi sasa ni mjamzito. Lakini mimi kila siku hasira zangu zinaongezeka na huenda wakati mwingine nikatukana na kulaani kwa sababu ya ndoa hii. Naomba kutoka kwa Shaykh maelezo na kuondosha kile kidukuduku na hasira iliyomo moyoni mwangu.

Jibu: Namwambia ndugu huyu atubu kwa Allaah na amuombe Allaah (´Azza wa Jall) msamaha. Usiingilie kati ya mtu na mke wake. Mwanaume huyu hakumuoa mwanamke huyu isipokuwa ilikuwa ni baada ya kupata idhini yake na yeye akaridhia hilo:

ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ

“Hiyo ni fadhilah ya Allaah, humpa amtakaye.”[1]

Ambaye kafanya mume kuwa bubu na mke mtamkaji ni Allaah (´Azza wa Jall). Usiwe ni mwenye kuamini mambo ya mkosi. Huenda watoto wa mwanamke huyu wakawa ni miongoni mwa watu walio wafaswaha zaidi na wenye kuzungumza vizuri zaidi. Kwa hivyo ni wajibu kwako kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) kutokana na yale yaliyotokea kwako katika kuapiza, kukasirika, kulaumu yaliyotokea na umuombe Allaah usalama juu ya watoto wa mwanamke huyu. Ambaye atamjengea dhana nzuri Allaah basi huyo yuko katika kheri.

[1] 57:21

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1041
  • Imechapishwa: 21/07/2020