Amekasirika akatoa talaka bila kutambua anachokisema

Swali 845: Kuna mwanaume aligombana pamoja na mkewe ugomvi mkubwa kabisa kwa kiasi cha kwamba akili yake ilibadilika ambapo akasema kumwambia mke wake: “Wewe nimekutaliki mara tatu”. Je, talaka imepita?

Jibu: Hali ikifikia kiasi cha kwamba haelewi kile anachokisema haipiti. Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 336
  • Imechapishwa: 17/08/2019