Amejiunga katika Rak´ah mbili za ´Ishaa na imamu na akatoa salamu pamoja naye

Swali: Tuliswali pamoja nawe swalah ya ´Ishaa na tulikuja katika swalah katika Sujuud ya kwanza ya Rak´ah ya pili ambapo tukaleta Takbiyr na kuswali kisha tukakaa pamoja nawe katika kikao cha Tashahhud ya kwanza. Kisha tukakamilisha Rak´ah mbili na wewe umeshatoa salamu na sisi tumesujudu sijda ya kusahau kabla ya kutoa salamu halafu ndio tukatoa salamu. Je, swalah zetu ni sahihi? Ikiwa sio sahihi ni lazima kuzirudi?

Jibu: Nilichofahamu kutoka katika maneno ya mwanamke huyu ni kwamba hakuswali isipokuwa tu Rak´ah mbili. Kwa hali yoyote ni kwamba ikiwa hakuswali zaidi ya Rak´ah mbili basi ni lazima hivi sasa arudi kuswali Rak´ah nne. Ama ikiwa alikamilisha Rak´ah mbili baada ya mimi kutoa salamu, basi ni lazima kwake kusujudu sijda ya kusahau baada ya salamu. Kama zimempita zimekwishampita na haimdhuru kitu.

Kwa kifupi ni kwamba ikiwa imamu analazimika kusujudu sijda ya kusahau baada ya kutoa salamu na baadhi ya watu wakalazimika kulipa baadhi ya Rak´ah wafanye vipi? Lililo la wajibu ni kwamba imamu akitoa salamu ya kumaliza swalah basi wanatakiwa kusimama na walipe zile Rak´ah wanazodaiwa. Jengine ikiwa amejiunga na imamu baada ya kusahau basi yeye atasujudu baada ya kutoa salamu. Ikiwa imamu alisahau kabla ya yeye kujiunga naye, hakuna kinachomlazimu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1594
  • Imechapishwa: 16/03/2020