Amejiharamishia kila anachomiliki – je, mke ameingia ndani?

Swali 850: Kuna mtu amejiharamishia kila kitu anachokimiliki. Je, mke wake anaharamika au hapana?

Jibu: Ama mbali na mke anatakiwa kutoa kafara ya yamini. Kuhusu mke wanachuoni wametofautiana kama ameachika na ni lazima kwake kutoa kafara ya kumfananisha mke na mama yake. Maalik anaona kuwa talaka imepita. Abu Haniyfah na ash-Shafi´iy katika maoni yaliyotangaa zaidi kwake wanaona kuwa anapaswa kutoa kafara ya yamini. Ahmad anaona kuwa analazimika kutoa kafara ya kumfananisha mke na mama isipokuwa ikiwa kama atanuia kinyume na hivo. Kwa hivyo ni jambo wanachuoni wametofautiana juu yake.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 337
  • Imechapishwa: 18/08/2019