Amejenga nyumba kwa pesa ya ribaa

Swali: Kuna mwanamke amejenga nyumba na pesa ya ribaa. Amepewa fatwa ya kwamba aiche nyumba na wala asiibomoe na badala yake atoe swadaqah kwa kiwango cha ile pesa aliyoijenga. Inajuzu kwake kumpa pesa hizi swadaqah dada yake ambaye ni fakiri?

Jibu: Ni nani aliyempa fatwa? Je, ni idara inayozingatiwa kwa fatwa? Katika hali hiyo aitendee kazi na ampe fakiri sawa akiwa ni dada yake fakiri au mwengine. Haitoi kwa njia ya kwamba ni swadaqah bali ni kwa njia ya kujikwamua na pesa ya ribaa. Asitegemee kupata thawabu kwa kitendo hicho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (5) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–01041434.mp3
  • Imechapishwa: 06/11/2016