Ameingia ndani ya ´ibaadah kwa kukusudia kujionyesha

Swali: Mtu akiingia ndani ya ´ibaadah hali ya kukusudia kujionyesha na kusifiwa. Kwa msemo mwingine mtu huyo hakukusudia kufanya ´ibaadah. Je, hiyo inakuwa shirki kubwa?

Jibu: Shirki ndogo. Kama ni muislamu inakuwa shirki ndogo. Kama Uislamu wa wanafiki ambao matendo yao yote yanakuwa ni unafiki na uwongo.

Swali: Baadhi ya wanazuoni wameigawanya shirki katika shirki ya nia, shirki ya matakwa na makusudio. Wamejengea hoja kwa Aayah isemayo:

مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لاَ يُبْخَسُونَ أُوْلَئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الآخِرَةِ إِلاَّ النَّارُ وَحَبِطَ مَا صَنَعُواْ فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُواْ يَعْمَلُونَ

”Anayetaka maisha ya dunia na mapambo yake, basi Tutawalipa kikamilifu matendo yao humo nao hawatopunjwa humo; [lakini] hao ndio wale ambao hawatokuwa na chochote katika Aakhirah isipokuwa Moto. Yataharibika yale yote waliyoyafanya humo [hapa duniani] na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.” (11:15)

Hapa ni pale ambapo atakusudia kwa Uislamu wake dunia. Kwa nia yake. Katika hali hiyo Uislamu wake ni batili. Ni kama Uislamu wa wanafiki. Lakini ambaye amesilimu kwa ajili ya Allaah na akamtakasia nia Allaah hata hivyo kujionyesha kukamtokea katika baadhi ya mambo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21909/حكم-من-اراد-بعبادته-الرياء-والمدح
  • Imechapishwa: 01/10/2022