Amehisi njaa sana akafungua katika funga ya jumatatu


Swali: Leo nimefunga jumatatu. Lakini baada ya alasiri wakati nilipoamka kutoka usingizini nikahisi kuchoka sana na sikuweza kukamilisha siku ambapo nikafungua. Je, nina dhambi katika hilo?

Jibu: Ikiwa ni swawm iliyopendekezwa hana dhambi. Ikiwa ni swawm ya wajibu ambapo ukafungua kwa sababu ya uzito, basi atatakiwa kuilipa. Ikiwa ni siku miongoni mwa masiku ya Ramadhaan, swawm ya nadhiri au kafara ambayo ni ya wajibu, basi haifai kwako kufungua isipokuwa kwa dharurah. Ukiwa hauna budi isipokuwa kula basi utafanya hivo kisha itakulazimu kuilipa siku nyingine. Ama ikiwa ni swawm iliyopendekezwa hakuna dhambi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 12/06/2019