Amegundua kasoro ya gari baada ya kuiendesha


Swali: Ikiwa muuzaji ataficha kasoro ya gari lake na mnunuzi akaigundua baada ya kuitumia…

Jibu: Ikiwa aliitumia pasi na kujua kasoro ya gari hiyo, basi ana haki ya kuirudisha kwa sababu hakuridhia hitilafu hiyo. Lakini ikiwa aliitumia baada ya kujua kasoro hiyo, basi hana haki ya kurudisha. Kwa sababu kuitumia kwake baada ya kutambua kasoro hiyo maana yake ni kwamba ameridhika nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (28)
  • Imechapishwa: 04/02/2022