Amegeuza nia kutoka siku sita za Shawwaal kwenda deni lake la Ramadhaan


Swali: Kuna ndugu mmoja alikuwa anadaiwa siku moja ya Ramadhaan. Ramadhaan ilipomalizika akasahau kuwa anadaiwa siku moja. Siku ya pil ya ´Iyd akafunga ambapo akanuia kufunga yale masiku sita ya Shawwaal. Ilipofida mida ya alasiri ndipo akakumbuka kuwa anadaiwa siku moja ambayo alazimika kuifunga ambapo akageuza nia kutoka ya sunnah na kwenda ya faradhi. Kisha akakamilisha swawm yake. Je, swawm yake hii inahesabiwa kuwa ni ya faradhi?

Jibu: Haihesabiwi kuwa ni faradhi. Hili tumelizungumzia punde tu. Tumesema kuwa  swawm ya faradhi lazima mtu atie nia kabla ya kuingia alfajiri. Kujengea juu ya hili tunamwambia ndugu muulizaji kwamba hivi sasa ni wajibu kwake kulipa siku anayodaiwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/950
  • Imechapishwa: 06/06/2018