Amefungua kwa kuchelea kuangamia kwa sababu ya kiu kikali

Swali: Katika Ramadhaan iliyopita nilizidiwa na kiu mpaka nikachelea kuangamia. Matokeo yake nikanywa maji kidogo. Je, nawajibika kulipa tu au ni lazima vilevile kutoa kafara? Ikiwa nalazimika kutoa kafara basi naomba uniwekee nayo wazi.

Jibu: Hulazimiki kutoa kafara katika hali kama hii. Shani ni katika kule kujuzu kufungua. Lakini hata hivyo muulizaji anasema kwamba alichelea kuangamia. Ikiwa kweli alichelea kuangamia basi inafaa kwake kufungua. Hapati dhambi. Halazimiki kutoa kafara. Kinachomlazimu ni yeye kulipa tu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=8PrwPENDLZg
  • Imechapishwa: 23/05/2018