Swali: Kuna mtu alitaka kumjamii mke wake mchana wa Ramadhaan ambapo akalazimika kufungua kwa makusudi kisha akamjamii mke wake pasi na yeye kuridhia jambo hilo. Ni kipi kinachowalazimu wote wawili?

Jibu: Mwanamme ni mwenye kupata dhambi kwa njia mbili:

1- Amepata dhambi kwa kufungua kwa makusudi. Kukusudia kufungua katika Ramadhaan ni dhambi kubwa. Hata imepokelewa kwamba yule mwenye kufungua siku miongoni mwa siku za Ramadhaan basi haitosihi kwake kuilipa hata kama atafunga mwaka mzima[1].

2- Kukiuka heshima ya mchana kwa kufanya jimaa. Kufanya jimaa mchana wa Ramadhaan ni kumuasi Allaah (Jalla wa ´Alaa).

Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah kwa kufungua kwake kwa makusudi na atubu kwa Allaah kwa kufanya jimaa mchana wa Ramadhaan. Ni lazima kwake kutoa kafara nzito; kuacha mtumwa huru, asipopata au akashindwa thamani yake basi afunge miezi miwili kamilifu mfululizo kwa ajili ya Allaah, asipoweza basi awalishe masikini sitini kwa kila siku moja aliyofanya jimaa. Hairuhusu akakimbilia kutoa chakula isipokuwa mpaka pale atakaposhindwa kufunga kutokana na ugonjwa au utuuzima. Allaah haimpi udhuru muda wa kuwa ni mwenye kuweza kufunga. Bali ni lazima kufunga miezi miwili mfululizo kwa sababu ya siku hiyo moja. Aidha atubu kwa Allaah na alipe siku hiyo. Asirudi tena katika kitendo mfano wa hicho huko mbeleni.

Mke wake akiwa ni mwenye kutenzwa nguvu – na Allaah ndiye anajua kama kweli alitenzwa nguvu – akajitetea lakini hata hivyo akamshinda, basi nataraji kuwa itamtosha kulipa siku hiyo.

[1] at-Tirmidhiy (723), Abu Daawuud (2396), Ibn Maajah (1672), Ahmad (02/470) na ad-Daarimiy (1714).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://mufti.af.org.sa/ar/content/%D8%B1%D8%AC%D9%84-%D8%A3%D9%81%D8%B7%D8%B1-%D8%AB%D9%85-%D8%AC%D8%A7%D9%85%D8%B9-%D8%B2%D9%88%D8%AC%D8%AA%D9%87
  • Imechapishwa: 01/05/2020