Swali: Kuna mtu aliulizwa juu ya kitu anachokijua ambapo akaapa kwa jina la Allaah kwamba hakijui. Hivi sasa anajuta sana kutokana na alichokifanya. Ni ipi kafara ya jambo hilo?

Jibu: Ni lazima kwake kutubu kwa kuficha elimu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuulizwa juu ya elimu akaificha, basi atapigwa hatamu ya Moto siku ya Qiyaamah.”

Isipokuwa tu pale ambapo mtu anachelea fitina na kuenea kwa shari kubwa juu ya kuelezea jambo hilo, katika hali hiyo ni mwenye kupewa udhuru. Hakika kuficha elimu ikiwa katika kufanya hivo kuna manufaa kubwa kuliko kuidhihirisha, basi hakuna neno kufanya hivo. Ni kama mfano wa ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Mu´aadh wakati alipomweleza haki ya waja kwa Allaah na haki ya Allaah kwa waja. Mu´aadh akamuuliza:

“Si niwabashirie watu?” Akamjibu: “Usiwabashirie wakabweteka.”

Kisha hatimaye Mu´aadh akabashirie hilo na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawabashiria watu hilo kwa lengo la kuwasimamishia hoja.

Kinacholengwa ni kwamba ikiwa kuelezea kwako jambo uliloulizwa kunapelekea katika shari ambayo ni kubwa na ya khatari, basi wewe ni mwenye kupewa udhuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9965/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D9%83%D8%AA%D9%85-%D8%B9%D9%84%D9%85%D8%A7
  • Imechapishwa: 03/05/2020