Ameenda katika nchi ambayo walichelewa kuanza Ramadhaan

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu ambaye amefunga na Saudi Arabia kisha akasafiri kwenda katika mji/nchi nyingine ambayo kulichelewa kwao kuingia kwa Ramadhaan. Je, mtu huyo afunge siku thelathini na moja?

Jibu: Afunge pamoja nao na afungue pamoja nao hata kama masiku yake yatazidi kutokana na Hadiyth iliyotangulia:

“Fungeni siku mnafunga, fungueni siku mnafungua.”[1]

[1] at-Tirmidhiy (697).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/155)
  • Imechapishwa: 16/05/2018