Swali 402: Mtu akichinja siku ya ´Iyd na akasahau kusema “Bismillaah”. Je, itafaa kwake kula katika kichinjwa hicho?

Jibu: Wanachuoni wengi wanaona kuwa itajuzu. Wako wengine wanaona kuwa hata kama hakutaja jina la Allaah, japokuwa atakuwa ni mwenye kukusudia, kichinjwa ni halali kwake. Miongoni mwao wako pia waliosema akisahau kichinjwa kwake ni halali na kama aliacha kusema kwa makusudi hapana. Kinachonidhihirikia ni kwamba akiacha kwa makusudi au akasahau basi asile kichinjwa chake. Kwa sababu Allaah (´Azza wa Jall) amesema katika Kitabu Chake kitukufu:

وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ

“Na wala msile katika ambavyo halikutajwa Jina la Allaah.”[1]

Kumebaki jambo, balo ni kwamba wanatumia dalili kwa Hadiyth ya ´Aaishah iliopo katika “as-Swahiyh” ya kwamba kuna watu walikuwa wakimletea nyama na wao ndio punde tu wametoka kwenye ukafiri na hawajui kama walitaka jina la Allaah au hawakutaja, kwa msemo mwingine watu hao wamekuwa waislamu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Tajeni [jina la Allaah] na kuleni.”

Tunaona hivi pale ambapo kichinjwa kitakuwa ni cha muislamu na akakupa nacho zawadi na wewe hujui kama alitaja jina la Allaah au hakutaja. Kimsingi ni kwamba muislamu husema “Kwa jina Allaah”. Lakini ukihakikisha kwamba hakutaja, basi kinachodhihirika ni kwamba kiache. Mwenye kuacha jambo kwa ajili ya Allaah basi humbadilishia bora kuliko hicho.

[1] 06:121

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 667
  • Imechapishwa: 02/02/2020