Amechelewesha kulipa siku zake za Ramadhaan kwa miaka tisa


Swali: Kuna mwanamke alipatwa na hedhi katika Ramadhaan na wala hakulipa siku zake isipokuwa baada ya miaka tisa kwa sababu ya ujinga wake. Je, kuna kinachomlazimu mbali na kulipa?

Jibu: Akiwa ni mjinga hakuna kinachomlazimu. Kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru. Jengine ni kwamba hakukusudia. Ikiwa atalipa pamoja vilevile na kulisha – kama walivyofutu baadhi ya Maswahabah wakubwa – hili ndio bora zaidi. Lakini inaweza kusemwa vilevile ya kwamba haiyumkiniki akakaa muda wote huu ilihali ni mjinga. Kwa sababu anaweza kuuliza. Akiwa ni muweza basi bora kwake ni yeye kulipa pamoja vilevile na kulisha. Ikiwa anadaiwa siku tano basi alishe kwa kila siku moja 1,5 kg chakula kinacholiwa katika mji. Ikiwa ni fakiri basi haimlazimu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (01) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=190884#219018
  • Imechapishwa: 29/12/2017