Amechelewesha Fajr hadi Dhuhr kwa kukosa mavazi na maji

Swali: Niliota na ukafika wakati wa swalah ya Fajr. Kutokana na kukosa nguo na ukali wa baridi sikuweza kuoga. Nikaacha kufanya hivo mpaka ukafika wakati wa Dhuhr ndipo niliweza kupata nguo na twahara. Ni ipi hukumu?

Jibu: Ilikuwa ni lazima kwake pale alipokosa maji ya moto na nguo afanye Tayammum kwa njia ya yeye kupiga mikono yake yote miwili kwenye mchanga kwa nia ya kuondosha janaba na kwa nia ya kuondosha hadathi ndogo ambayo ni kufanya wudhuu´. Kisha afute uso wake na viganja vyake vya mikono hali ya kuwa ni mwenye kunuia janaba na wudhuu´ yote mawili. Baada ya hapo aswali kwa kiasi cha hali yake. Haifai kwake kuchelewesha swalah hata siku moja. Akiichelewesha anapata dhambi. Katika hali hiyo itamlazimu kwake kuoga na kulipa swalah aliokuwa anadaiwa. Lakini ilikuwa inamlazimu kuswali ndani ya wakati wake ijapokuwa ni kwa kufanya Tayammum. Akiweza kuyachemsha maji na kupata nguo itayomsaidia kumsitiri basi itakuwa ni wajibu kwake. Vinginevyo ataswali kwa kufanya Tayammum na wala asicheleweshi swalah nje ya wakati wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3796/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D8%AE%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%BA%D8%B3%D9%84-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D9%84%D8%B4%D8%AF%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%A8%D8%B1%D8%AF
  • Imechapishwa: 22/03/2020